KUHUSU KITUO
Karibu Sana
Karibu Kutonarweza kituo kizuri na cha kisasa cha kulea watoto. Kituo kilisajiliwa mwaka 2017 kwa mujibu wa sheria na taratibu za wizara husika. Namba ya usajili ni 1176. Kituo hiki kinapatikana eneo la Swaswa Mashineni mkabala na kanisa Katoliki la Swaswa.
Kituo chetu kinajivunia kuwa katika mazingira tulivu isio na kelele za magari au karakana yoyote hivyo huwapa watoto fursa ya kuwa katika hali ya utulivu.


